Wednesday, 2 September 2009

Zanzibar State University.


Licha ya kuwa elimu bora sio majengo bora na wala sio uzuri wa majengo lakini ni vyema hasa ikiwa mnaishi katika ulimwengu wa wastaarabu mkajitahidi angalau kuwa na majengo yaliyomauri na yaliyopo katika maeneo muwafaka.

Sijui wenzangu mnalitazamaje suala la chuo kikuu cha taifa SUZA kuwepo katika eneo hili la mjini lisilo hata na nafasi nzuri ya kieneo.

Nnavyofahamu mimi ni vyema tukapata sehemu nzuri ambayo itasaidia wasomi wetu kupata sehemu ya mapumziko na kujadili masomo yao. Katika nchi za wenzetu ni kweli kuwa wana vyuo vikuu mijini lakini wanazingatia pia suala la utulivu na eneo kubwa kwa wanachuo ili wapate wapumzike na kutafakari.

Kwa hapa kwetu chuo hiki kilichopo hapa sioni kama ni busara na ikiwezekana ni vyema basi serikali ikakitafutia sehemu nyingine ya kukijenga kuliko hapa kilipo hivi sasa.

No comments:

Post a Comment