Wednesday, 2 September 2009

Baada ya Muda wa ukimya.



Nimejaribu kwa kiasi kikubwa kufikiria ni jinso gani nnaweza nikayatekeleza maoni ya wadau wangu wa Blogu hii, kwa kunitaka nitumie zaidi lugha ya kiswahili, Na hatimae hivi leo nimeona nianze kwa kukidhi haja ya wadau hao.

leo hii hebu tuone vitu viwili ambavyo ni muhimu sana kwa wadau kujua. idara ya Mazingira imekuwa ikipiga kelele kwa siku nyingi sana suala la kuweka mazingira yetu safi yanayotuzunguuka lakini cha kushangaza si wao idara hiyo, wala Baraza la Manispaa vilivyodiriki kuliona ama hata kama wameliona lakini hatua zinazofaa haziwahi hata siku moja kuchukuliwa ili kulipiga marufuku tendo hili lakuchukua boti kutoka baharini na kuja kuziweka katika makaazi ya watu.

Boti hii ipo maeneo ya Bweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar, lakini eneo hili pia ndilo eneo linalotarajiwa kuwepo baraza la Wawakilishi kwa siku zijazo. Si hayo tu lakini hata chuo cha Afya cha Zanzibar kipo katika maeneo haya.

hizi picha tofauti zinaonyesha jinso mmiliki ambae tumeshindwa kumjua alivyoiweka boti hii inayokadiriwa kutumia zaidi ya miaka mitatu eneo hili.

Chini ya boti hii kuna wadudu hatari wameshaweka maskani wakiwemo nyoka na pia eneo hili sasa limekuwa hatari kwa watoto wa eneo hili la Mbweni kucheza katika eneo hili.

Lakini ni kitu gani na hatua zipi zitachukuliwa na Idara zinazohusika, hebu tuangalie kama hilo litawezekana.

No comments:

Post a Comment