Sunday, 27 September 2009

My Radio Logo.


This is my Radio Logo. Ni kama ujuavyo kila Radio ni vizuri ikwa na alama yake na sisi tumeitengeneza hii tangu kuanza kwa Radio yetu na ndio inayotumika kututambilisha katika sehemu kadhaa.

Wednesday, 16 September 2009

Trafic lightlong time not working.


Hizi ni taa za bara barani katika eneo la mkunazini, taa hizi zina karibu mwezi mmoja hivi sasa haziwaki hivyo kuwa kero kwa watumiaji wa sehemu hii.
Na sio sehemu hii tu, hata eneo la Malindi chini ya kituo kikuu cha polisi wa bara barani pia taa zake zina karinu miezi minne haziwaki.
Nadhani hatua za dharura zinahitajika kuchukuliwa ili kuepusha maafa kufuatia kukosekana kwa taa hizi.

in the Meeting at Zenji Fm.

Andrea Schmidt she seems to be very happy because of good agreements, while Sevan seems to be very intrest with the topic in the meeting with Zenji Fm leaders.

Here was in the office at Mombasa in Zanzibar where Zenji Fm is located now days..

I hope what we achive together in the meeting will work and we will all keep our realation.

Deutsche Welle and Zenji Fm.


From the left is Sevan Ibrahim a Deutsche Welle, Project Manager Distribution Africa/middle East , Centre is Issa Msabah Zenji Fm Radio Assistance Enginier and the right Side is Andrea Schmidt, when they are at Masingini Area where Zenji Fm radio has its Transmiter.
These two leaders was in Zanzibar for talking with our Radio leaders and to review some agreaments.

Friday, 4 September 2009

Ni picha za Forodhani.




Kwa kuwa ni muhimu kuziona hizi picha na ptazamo wake wa hivi sasa. Nimeona ni vyema nikaazituma na picha nyingine zaidi ambazo nilibahatika kuzichukua katika eneo hili la Forodhani.




Kwa kuwa nnamjali sana Hariet Jasson aliyetaka niziweke picha hizi nimeamua kufanya hii kazi kwa niaba yake na hivi sasa nnaziweka ili kila ambae anahitaji kuiona mandhari hii mpya aweze kufanya hivyo.




Na ikiwa mtu yoyote ana maoni juu ya mandhari hii anaweza akanitumia maoni hayo kupitia katika Blog yangu hii.


Kwa kuwa mazingira ni yetu sote naomba tulitunze eneo hili na ikiwa serikali ina uwezo mwengine basi hata Jamhuri Garden itengenezwe ifanane na hii ya Forodhani.

New forodhani Garden View.




Kumbe watanzania tunapokusudia kufanya kitu huwa tunaweza lakini ni watu wachache mno ndio wanaotukwaza katika kuyimiza lile tunalolitaka.




Katika eneo la forodhani kulikuwa na eneo ambalo lilikuwa ni maarufa kwa wananchi kufika nyakati za usiku na kufurahika kwa kununua chakula na kupumzika.




Vyakula vya ainda nyingi sana vilikuwa vikipatikana lakini baada ya kuonekana umuhimu wa eneo hilo Serikali imeamua kuifanyia matengenezo eneo hilo na kujenga bustani ambayo kwa hivi sasa imekuwa ni kivutio kikubwa sana kwa wageni na wananchi wenyewe.




Hizi ni baadhi ya picha zinazoonyesha eneo labustani ya Forodhani.

Wednesday, 2 September 2009

Zanzibar State University.


Licha ya kuwa elimu bora sio majengo bora na wala sio uzuri wa majengo lakini ni vyema hasa ikiwa mnaishi katika ulimwengu wa wastaarabu mkajitahidi angalau kuwa na majengo yaliyomauri na yaliyopo katika maeneo muwafaka.

Sijui wenzangu mnalitazamaje suala la chuo kikuu cha taifa SUZA kuwepo katika eneo hili la mjini lisilo hata na nafasi nzuri ya kieneo.

Nnavyofahamu mimi ni vyema tukapata sehemu nzuri ambayo itasaidia wasomi wetu kupata sehemu ya mapumziko na kujadili masomo yao. Katika nchi za wenzetu ni kweli kuwa wana vyuo vikuu mijini lakini wanazingatia pia suala la utulivu na eneo kubwa kwa wanachuo ili wapate wapumzike na kutafakari.

Kwa hapa kwetu chuo hiki kilichopo hapa sioni kama ni busara na ikiwezekana ni vyema basi serikali ikakitafutia sehemu nyingine ya kukijenga kuliko hapa kilipo hivi sasa.

Baada ya Muda wa ukimya.



Nimejaribu kwa kiasi kikubwa kufikiria ni jinso gani nnaweza nikayatekeleza maoni ya wadau wangu wa Blogu hii, kwa kunitaka nitumie zaidi lugha ya kiswahili, Na hatimae hivi leo nimeona nianze kwa kukidhi haja ya wadau hao.

leo hii hebu tuone vitu viwili ambavyo ni muhimu sana kwa wadau kujua. idara ya Mazingira imekuwa ikipiga kelele kwa siku nyingi sana suala la kuweka mazingira yetu safi yanayotuzunguuka lakini cha kushangaza si wao idara hiyo, wala Baraza la Manispaa vilivyodiriki kuliona ama hata kama wameliona lakini hatua zinazofaa haziwahi hata siku moja kuchukuliwa ili kulipiga marufuku tendo hili lakuchukua boti kutoka baharini na kuja kuziweka katika makaazi ya watu.

Boti hii ipo maeneo ya Bweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar, lakini eneo hili pia ndilo eneo linalotarajiwa kuwepo baraza la Wawakilishi kwa siku zijazo. Si hayo tu lakini hata chuo cha Afya cha Zanzibar kipo katika maeneo haya.

hizi picha tofauti zinaonyesha jinso mmiliki ambae tumeshindwa kumjua alivyoiweka boti hii inayokadiriwa kutumia zaidi ya miaka mitatu eneo hili.

Chini ya boti hii kuna wadudu hatari wameshaweka maskani wakiwemo nyoka na pia eneo hili sasa limekuwa hatari kwa watoto wa eneo hili la Mbweni kucheza katika eneo hili.

Lakini ni kitu gani na hatua zipi zitachukuliwa na Idara zinazohusika, hebu tuangalie kama hilo litawezekana.