Thursday, 17 June 2010

MTAMBO WA GESI UTOKANAO NA TAKA. TAKA



Wenzetu kule jijini Dar es salaam kwa siku nyingi tu maeneo ya Mtoni Kwa Azizi Ali, sehemu ambayo ilikuwa na jaa la taka taka wametengeneza mtambo wa kuzalisha gesi ili kuzuia uchafuzi wa mazingira.

Licha ya kwamba gesi hiyo bado haijaanza kufanyiwa kazi muhimu lakini kwa kiasi kikubwa mno wameacha kuchafua mazingira kwa kuiunguza ile gesi ambayo inazalishwa kutoka katika eneo hilo lililokuwa maarugu kwa uchafuzi huo wa mazingira.

Nalo baraza la manispaa la Zanzibar linampango wa kufanya hivyo katika jaa lake lililopo Jumbi nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

hizi ni baadhi tu ya picha za mtambo huo uliopo jijini Dar es salaam kwa Aziz Ali.

No comments:

Post a Comment