Thursday, 17 June 2010
MTAMBO WA GESI UTOKANAO NA TAKA. TAKA
Wenzetu kule jijini Dar es salaam kwa siku nyingi tu maeneo ya Mtoni Kwa Azizi Ali, sehemu ambayo ilikuwa na jaa la taka taka wametengeneza mtambo wa kuzalisha gesi ili kuzuia uchafuzi wa mazingira.
Licha ya kwamba gesi hiyo bado haijaanza kufanyiwa kazi muhimu lakini kwa kiasi kikubwa mno wameacha kuchafua mazingira kwa kuiunguza ile gesi ambayo inazalishwa kutoka katika eneo hilo lililokuwa maarugu kwa uchafuzi huo wa mazingira.
Nalo baraza la manispaa la Zanzibar linampango wa kufanya hivyo katika jaa lake lililopo Jumbi nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
hizi ni baadhi tu ya picha za mtambo huo uliopo jijini Dar es salaam kwa Aziz Ali.
Thursday, 10 June 2010
Nusu Mwaka imekwisha.
Tumeingia kwenye mwezi wa sita ni nusu ya Mwaka hivyo naamini nusu ya matarajio na malengo yetu huenda yakawa yametimia. Sasa tunakwenda kwenye sehemu nyingine ya mwaka. Swali Jee! Tumejiandaaje? Unaponiona naelekea kwenye nusu mwaka iliyobakia tena nikiwa na haraka kubwa sana. Huko nnakokwenda kuna uchaguzi mkuu wa Tanzania, serikali ya pamoja ya SMZ na hivi karibuni naanza na kombe la dunia litakalofanyika kwa mara ya kwanza Barani Afrika.
Naamini tutafika pamoja, kwa hivyo tuwe sote.
Heri ya nusu mwaka.
Subscribe to:
Posts (Atom)